Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Seyyid Ebrahim Raisi ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki.
Katika mazungumzo hayo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uwezo na fursa zilizopo za kustawisha mahusiano na mashirikiano kati ya Tehran na Ankara katika nyanja za pande mbili na za kikanda na akasema, Iran inakaribisha uandaaji ratiba na mipango ya ushirikiano wa kistratejia na Uturuki.
Aidha, amesisitizia ulazima wa kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi za nchi zote, akisema ndio njia pekee ya kudhamini usalama na uthabiti endelevu katika sehemu mbalimbali za eneo.
Kwa upande wake, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema nchi yake imeandaa orodha ya masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi kwa ajili ya kuimarisha na kustawisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akabainisha hamu aliyonayo ya kuitembelea Tehran hivi karibuni.
Katika mazungumzo hayo ya simu, Erdoğan ametilia mkazo pia kuendelezwa upatikanaji wa nishati kutoka Iran kwa ajili ya Uturuki na akaongeza kuwa, Uturuki inaitambua Iran kuwa ni mdhamini wa uhakika wa nishati na inataka kuongezwa kiwango cha mashirikiano yake na Tehran.
Rais wa Uturuki amemalizia kwa kusisitizia msimamo wa nchi yake wa kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kudhamini usalama wa eneo.../
342/